DC MAGOTI: KIJANA HUJAPATÀ ENEO LA KILIMO? Ni-dm Instagram


                             

                                                   Na Mwandishi Wetu, Kisarawe Pwani.

MKUU wa Wilaya Kisarawe, Petro Magoti amewataka vijana ambao bado hawajapata maeneo ya kilimo, wamtumie ujumbe wa maneno ‘DC Sijapewa eneo la kilimo’ katika Instagram yake petromagoti.

Akizungumza 13 Januari 2026 wakati wa ziara ya kukagua maeneo waliyopewa vijana kwa ajili ya kilimo na kuacha kukaa kijiweni, wilayani humo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kulingana na utafiti aliofanya na kuzungumza na wenyeviti wa vijiji maeneo bado yapo.


Kisarawe tuna eneo kubwa sana kwa kilimo na hakuna ukame mvua ni mara mbili kwa mwaka” alisema na kuongeza kuwa hakuna kijana kukaa kijiweni na kucheza pool muda wa saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana kwani muda huo ni wa kazi na atakayebainika atamueleza anaishije.

“Utanieleza, unalipaje bili ya maji, umeme unakula, kulaje sababu kutwa nzima upo stendi na wale ambao mnasema hamna maeneo mnakuja kupewa eka mbili” alisema na kuongeza kuwa trekta lipo limeletwa wilayani humo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Alisema hakuna kijana kukaa kijiweni  na anawabainisha wanadai kuwa anawapangiaje kazi kuwa hilo ni agizo la serikali hakuna kuhoji asiye nalo awasiliane nae.

Alisema atafanya ukaguzi kila sehemu kuhakikisha agizo la kutocheza Pool muda wa kazi na pia ameagiza watoto wenye ulemavu wapelekwe shuleni kuandikishwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema amewaagiza wakuu wa shule, walimu wakuu na maofisa elimu msingi na sekondari kuwapokea wanafunzi hata kama vifaa wanavyotakiwa kuwa navyo havijakamilika.

“Hata kama mtoto hana sare za shule apokelewe na mzazi apewe muda wa kukamilisha kwani sare sio zinazosoma ni utambulisho tu wa mwanafunzi” alisema.

Magoti amewataka wazazi wasio na uwezo kuonana nae ofisini kwake kujadiliana na kusisitiza awe kweli hana uwezo ikibainika ameongopa atachukuliwa hatua  ikiwa ni pamoja na kupewa adhabu ya kulimishwa shamba lenye ukubwa wa ekari tatu.



 

Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA