17 WAPATA MSAMAHA WA RAIS CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR
RAIS Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo 11 Januari ametoa msamaha kwa wanafunzi (wafungwa) 17 wa liokuwa Chuo cha Mafunzo Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi.
Taarifa ya Ikulu Zanzibar iliyosainiwa na Naibu Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, Mohamed Raqey ilisema kwa mujibu wa Mamlaka aliyopewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi chini ya kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 cha kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kwa kosa lolote.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ametumia mamlaka hayo kikatiba msamaha katika kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar" ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Ikulu, Zanzibar.
Katika msamaha huo taarifa imetaja idadi ya wanafunzi 17 waliopewa msamaha wa kutumikia adhabu zao na kuachiwa huru na kati yao 11 ni wa Unguja na sita ni wa Pemba.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida wa Rais wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutoa msamaha kwa baadhi ya wanafunzi (wafungwa) wa chuo cha mafunzo wakati wa maadhimisho kiTaifa kama haya.

Comments
Post a Comment