NCCR Mageuzi haitambui 'No Reform, No Election"

 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimetangaza kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu 2025 na hakitambui kitu kinachoitwa ‘No Reform, No Election’.

Akizungumza katika mahojiano mara baada ya kutangazwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho leo 29 Machi 2025 mjini Dodoma kuwa mgombea Urais kupitia chama hicho, Haji Ambar Khamis alisema wanashiriki uchaguzi mkuu kikamilifu.

Alisema suala la uchaguzi mkuu ni la kikatiba na mtu yeyote akivunja katiba ni uhaini na wao NCCR Mageuzi hawapo tayari kufanya hivvyo.

“Hatupo tayari kuvunja katiba yetu wala ya chama na hata hayo maendeleo utayadai vipi kama usiposhiriki uchaguzi mkuu?” alihoji,

Joseph Selasini, ambaye amechaguliwa kuwa mgombea Mwenza alisema anasikia kuna watu wanasema “No Reform, No Election” wao NCCR Mageuzi hawaelewi.

“Hatuelewi, wala hatujaelimishwa hivyo tutaendelea kuhubiri uchaguzi mkuu” alisema Selasini.



Comments

Popular posts from this blog

CCM YAISHUKURU SMZ, WAKAZI KIKWAJUNI

CCM YAONYA WATEULE MIUNDOMBINU ZANZIBAR

TRA YATAKIWA IJIPANGE DIRA MAENDELEO YA TAIFA